Tuesday, 1 October 2013

KWA NINI MANCHESTER UNITED IPO KWENYE HALI HII YA SASA???


Robin Van Persie kushoto,Michael Carrick katikati na Wyne Rooney.
MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER United ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Imefungwa mechi tatu kati ya sita za mwanzo wa msimu huu na haijafunga bao lolote kwa soka la kutandaza tangu ilipoishinda Swansea zaidi ya wiki sita zilizopita.
Huu ni mwanzo mbaya zaidi wa timu hiyo kwenye ligi baada ya miaka 25 kupita. Haijatokea hivyo tangu Manchester United ya Sir Alex Ferguson ilipouanza msimu wa 1989/1990 walipokuwa na pointi saba baada ya mechi sita.
Hizo ni takwimu zinazoihusu Manchester United kwa sasa. Kocha mpya David Moyes anasugua kichwa, mashabiki nao hawaelewi, huku kelele za kuzomea baada ya filimbi ya mwisho kwenye mechi ya kipigo cha 2-1 kutoka West Bromwich Albion zikifungua zama mbaya zaidi.
Nafasi ya 12 kwenye ligi
Mara ya mwisho Manchester United kushika nafasi hiyo au kuwa chini ya hapo baada ya mechi sita ilikuwa mwaka 1986. Kipindi hicho, Manchester United ilikuwa chini ya kocha Ron Atkinson na timu hiyo iliporomoka hadi nafasi ya 19.
Ferguson aitwa kuokoa jahazi
Hali ya timu ilikuwa mbaya, ilikuwa inaelekea kushuka daraja. Mabosi wa Manchester United walifanya uamuzi na kumwita Alex Ferguson kikosini. Ferguson alitua kwenye timu hiyo na kunusuru hali ya mambo.
Jumamosi iliyopita, mashabiki wa Old Trafford waliishia kuimba tu jina la Sir Alex Ferguson ambaye kwa sasa ameamua kulipa kisogo soka. Kila kitu kimekuwa historia.
Hata hivyo, wakati Manchester United ikiwa chini ya Moyes, kuna kitu hakipo sawa kwenye timu hiyo na kuwafanya mabingwa hao kushika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi.
Matatizo ya usajili na viungo dhaifu
Kushindwa kuchukua hatua kwenye kipindi cha usajili ndicho kinachofichua tatizo la kiungo dhaifu kwenye kikosi hicho cha Manchester United kwa sasa.

No comments:

Post a Comment