Wednesday 4 September 2013

SOMA LIST YA NYIMBO 10 BORA ZA INDIA MUDA WOTE



latamangeshkarsinging.jpg
Mangeshkar

Nyimbo au music ni kila kitu katika maisha ya watu wa India,ni zaidi ya soka kwa watu wa Brazil,ni zaidi ya Basketball kwa watu wa Marekani.Unapomzungumzia binti mzuri wa kihindi lazima uizungumzie..
sauti nzuri ya kuimba,lazima uzungumzie uwezo mzuri wa kupenda unaochchowa na uwezo wa kuimba nyimbo zenye hisia za mapenzi,zinaweza zikawa za huzun au za furaha.Lakini zaidi ya yote panapokuwa na watu wanaoweza jambo fulani basi wapo wanaoweza zaidi na hata kuwa watu maarufu kwa kitu wanachokifanya.Leo nakuletea listi ya nyinmbo kumi bora kutoka kwa mwimbaji maarufu India.listi ya nyimbo hizi zimetokana na kura zilizopigwa na washabiki wa music inchini India kupitia mtandao wa Bollywood na kuchagua nyimbo 10 bora za muda wote katka maisha ya watu wa India zikiimbwa na waimbaji bora wa muda wote wa Historia ya music India,Mangeshka na  Asha Bhosle.

1. Tu jahan jahan chalega (Mera Saaya, 1966). Music: Madan Mohan. Lyrics: Raja Mehdi Ali Khan.Wimbo huu unazungumzia hisia kubwa anazozipata mtu baada ya kuwa anamhitaji mtu aliekuwa anampenda wakati anapompoteza.
2. Lag jaa gale (Woh Kaun Thi, 1964). Music: Madan Mohan. Lyrics: Raja Mehdi Ali Khan.Wimbo huu unazungumzia ni kwa namna gani mapenzi yanaweza yakaiteka akili ya mtu.
3. Aaja re pardesi (Madhumati, 1958) Music: Salil Chowdhury. Lyrics: Shailendra.Wimbo huu unazungumzia ni kwa namna gani music unaishi katika moyo wa mtu
4. Rahe na rahe hum (Mamta, 1966) Music: Roshan Lyrics: Majrooh Sultanpuri.wimbo huu unazungumzia utungaji wa mashairi ya kuvutia.
5. Ja re ud jaare panchi (Maya, 1961) Music: Salil Chowdhury. Lyrics: Majrooh Sultanpur.wimbo huu unazungumzia jinsi mapenzi yanavyoweza kuugusa moyo.
6. O sajna, barkha bahaar aayi (Parakh 1960). Music: Salil Chowdhury. Lyrics: Shailendra.wimbo huu unazungumzia umuhimu wa mvua katika mapenzi.unapokuwa na mpenzi wako alafu mvua ikanyesha inamaanisha nini?
7. Aaega aanewala (Mahal, 1949). Music: Khemchand Prakash. Lyrics: Nakhshab Jaaravch.wimbo huu unaelezea ni kwa namna gani furaha ya mtu inaweza kuongezeka baada ya kupata furaha ya mtu mwingine.
8. Pyaar kiya toh darna kya (Mughal-e-Azam, 1960). Music: Naushad. Lyrics: Shakeel Badayun.wimbo huu unazungumzia hisia mbalimbali zinazoweza kutokea zikisababishwa na nyakati au kipindi fulani cha maisha ya mtu.
9. Allah tero naam (Hum Dono, 1961). Music: Jaidev. Lyrics: Sahir Ludhianviwimbo huu unatoa mashahiri muhumu kwa ajii ya kumpa tumaini mpenzi umpendae katika maisha yako.
10. Zara si aahat hoti (Haqeeqat, 1964). Music: Madan Mohan. Lyrics: Kaifi Azmi.wimbo huu unazungumzia hisia za utulivu anazozihitaji mtu wakati wa kusikilza nyimbo.

No comments:

Post a Comment