Thursday 5 June 2014

PIQUE;FABREGAS ALINIAMBIA ATAONDOKA

Fabregas told me 'he's off', says Pique

Kocha Maximo rasmi Yanga


0
Share


WAPINZANI wote wa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara wakisikia hii lazima wakatangaze. Mwenyekiti wa timu hiyo Yusuf Manji amekubali kugombea tena kwenye uchaguzi ujao.Lakini hiyo siyo tamu sana, kali ni kwamba ametamka kwa mdomo wake mbele ya mamia ya wanachama jijini Dar es Salaam kwamba Mbrazili, Marcio Maximo aliyejenga heshima ya Taifa Stars na soka la Tanzania,  ndiye kocha mkuu mpya wa Yanga.
Akitumia dakika 31 katika hotuba yake ya awali kwenye mkutano mkuu wa Yanga uliofanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la maofisa wa Polisi, Osterbay, jana Jumapili, Manji alitangaza msimamo wake wa kutogombea na kuthibitisha ujio wa Maximo. Lakini baadaye akahamasishwa na kubadili mawazo.
Katika mkutano huo wa dharura uliokuwa na agenda moja ya mabadiliko ya Katiba, alisema: “Tunamalizia mazungumzo katika mambo madogo ya maslahi, nathibitisha rasmi kwamba atakuja hapa, nataka kumleta Maximo ili aendane na hadhi ya Yanga hatuna matatizo naye anatuelewa vizuri na sisi tunamjua ni rafiki yetu wanachama tulieni.
“Kuhusu usajili wa timu, tumebakiza wiki mbili kumalizia kamati ya usajili inaendelea na kazi hiyo, hatutaki kusajili wachezaji wengi tutasajili wachezaji watatu wa ndani na wawili kutoka nje, kikosi chetu si kibaya tunafanya kujazia tu, tumemfunga Al Ahly hapa kwetu hiyo sio timu mbovu hata kidogo hata hili la kijana wetu Okwi (Emmanuel) tutalimaliza hakuna shida.”
Mara baada ya kumalizika kwa majadiliano ya mabadiliko ya katiba ambayo yote yalipita kama ilivyotakiwa, ilipofika katika kipengele cha mengineyo wanachama wa Yanga waliibua hoja upya ya Manji kutogombea tena ambapo kwa pamoja walisimama na kusema hawakubaliani jambo ambalo lilianzisha mchakato mwingine mpya.
Hoja hiyo iliibuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Yanga Mzee Jabir Katundu ambapo baada ya wanachama kutoa msimamo huo ilimlazimu Manji kuomba ridhaa ya yeye na kamati yake ya utendaji kutoka nje ya ukumbi na kuwaachia wanachama hao kujadiliana kwa uhuru ambapo msimamo ulibaki uleule kuwa aendelee kwa miaka minne ijayo.
Kufuatia msimamo huo Manji aliporudi alipewa majibu hayo na yeye kuombwa aongoze kwa mwaka mmoja zaidi baada ya wanachama wa Yanga kubariki kubadilishwa kwa tarehe ya mkutano mkuu wa uchaguzi ambao sasa utafanyika Juni 14 mwakani.
“Lengo letu la kubadilisha tarehe ya uchaguzi ni kwa vile hatutaki kuleta vurugu katika timu yetu kwa sasa kupitia uchaguzi mkuu kama ambavyo inaendelea kwa wenzetu sasa, endapo tutafanya uchaguzi mwaka huu ni wazi utaangukia katika kipindi cha mashindano, nitaendelea mpaka mwakani lakini pia kipindi hiki nitakuwa nafikiria kwa kina kuhusu hili ni lazima nizungume na familia yangu,”alisema.
Katika hatua nyingine Manji alizungumzia suala la ujenzi wa uwanja wao ambapo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick kwa kutoa jibu la kupatikana kwa eneo la ujenzi na kuwashawishi wanachama kutowapa kura madiwani watakaobainika kukwamisha mpango huo.

Mechi tano kali zaidi kwenye Kombe la Dunia

TFF kusikiliza rufaa ya Wambura