SAKATA la Uchaguzi Mkuu wa Simba limeingia katika hatua nyingine ambapo Kamati ya rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inaketi Jumatatu ya Juni 9, mwaka huu kusikiliza rufani iliyowekwa na Michael Wambura.
Rufani hiyo iliwekwa na Wambura aliyekuwa anawania
nafasi ya makamu wa rais kupinga kuondolewa kwake katika kinyang’anyiro
hicho na Kamati ya Uchaguzi ya Simba.
Wambura anapinga kuondolewa katika nafasi hiyo
kutokana kwa sababu ya kutokidhi vigezo vya kugombea ikiwemo kutokuwa
mwanachama wa Simba.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa
na Wakili Julius Lugaziya itakutana saa 5, asubuhi kwenye Hoteli ya
Courtyard iliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam kujadili rufani hiyo na
kutoa matokeo.
Wakati huohuo, wachezaji wawili Ali Shabani Mabuyu
na Juma Yusuf waliochaguliwa kwenda kwenye kambi ya Copa Coca-Cola ya
Dunia nchini Brazil jana wamekabidhiwa bendera tayari kwa safari hiyo.
No comments:
Post a Comment