Thursday 15 May 2014

Neymar aibua balaa



VITA kubwa imeibuka kati ya klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil kuhusu supastaa Neymar.
Miamba ya soka Hispania, Barcelona wanataka kumtumia Mbrazili huyo kwenye mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi Kuu Hispania wakiamini watashinda ili kunyakua ubingwa, wakati Brazil hawataki acheze kwa hofu ya anaweza kuumia kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia kwa sababu ndiye tumaini lao kubwa.
Barca wanataka Neymar acheze kwa sababu ndiye mchezaji pekee aliyefunga bao walipomenyana na Atletico msimu huu na hivyo wanamini ataendeleza makali yake dhidi ya kikosi hicho kinachonolewa na Muargentina Diego Simeone.
Chama cha soka Brazil na wadhamini wa supastaa huyo hawataki acheze kwa sababu jambo hilo linaweza kumsababishia majeruhi yatakayomfanya akose fainali za Kombe la Dunia.
Nchini Brazil, Neymar si mchezaji wa kawaida tu, bali ni kipenzi kikubwa wa vyombo vya habari vya nchi hiyo na kwamba makampuni mengi yamekuwa yakicheza kamari kuhakikisha staa huyo anakuwapo kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazoanza mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment