Arsene Wenger |
Ugumu wa
moyo wa Mohamed Ghadafi ulisababisha kuuawa na majeshi ya NATO huku nafsi yake
ikitamani kuendelea kuishi.Ugumu wa moyo wa Adolph Hitler umeiachia dunia
maswali mengi....
kuwa yupo hai au ameshakufa na hata kama amekufa nini kimemuua
hakuna mwenye uhakika hata wazungu wameishia kuatabiri tu!
Wakati
Wenger anakuja Arsenal msimu wa 1996 na kutokufanya vizuri katika msimu huo wa
mwanzo kila mtu aliamini moyoni mwake huyu mtu mrefu na akili zake zitakuw
andefu hivyo na malengo yake yatakuwa malengo yake yatakuwa ya muda mrefu basi
hata mafanikio yatakuwa ya muda mrefu pindi atakapoaanza kufanikiwa .Kila mtu
alimuona amerukwa n akili pale alipomuuza Nicolas Anelka kwenda Real Madrid na
kumsajili Tiery Henry kutoka Juventus tena sio Henry aliendoka Arsenal
bali ni Tiery aliekuwa anakaa benchi
Juve.
Baada ya
hapo akaaznza kuitengeneza Arsenal mpya Arsenal ya Viera,Timu yenye ukuta wa
Berlin chini ya Tom Adams kisha kumpa kijiti Sol Cambel ndipo mashabiki
wakaanza kubeba mabango yaliyoandikwa WE BELIVE IN WENGER.Kila mshabiki
alimuona yeye ni kama imani ya kumfikisha katika mbingu ya Highbury.
Hapo hata kama
ningekuwa ni mimi ningemwamini,kwa nini nisimwamini mtu anacheza mechi 49
mfululizo bila kufungwa mchezo hata mmoja tena katika ligi ngumu kama ya
Uingereza,kwa nini nisimwamini mtu aliemtoa Thiery Henry kwenye benchi la
Juventus na kuwa mungu mtu pale Arsenal,mtu aliemtoa Viera kutoka mtu wa
kawaida hadi shujaa.
Wenger ndie
alieanzisha mfumo wa kuwaleta wachezaji wajanja na wepesi kwenye ligi ya
Uingereza,viungo wa ugali na akili nyingi kkkama Viera,hiyo ndio iliyokuwaa
siri ya mafanikio ya Wenger kwa Arsenal isiyofungika.maisha yanakwenda kwa kasi
hivyo hata mambo yanabadilika kwa kasi sana,kaktika mpira wa sasa ni tofauti na
wazamani,kama usipokuwa na kiasi kikubwa c ha pesa huwezi kupata wachezaji wa kiwango ch dunia kama akina
Mesi,Ronaldo,Bale Suarez na wengine.
Wakati
Wenger anawanunua akina Thiery na
Viera leo gharama alizotumia hazitoshi
kuwanunua akina Diady na Welbeck.Akili ya Wenger na maazo yake yalijaribu
kuwaza mbali na kufikiria baada ya Viera na Henry kuondoka nani watarithi
nafasi zao,akapiga mahesabu na yakaja na kuanza kuandaa kizazi kipya kuitangaza
Arsenal nyingine ,taratibu akamleta Cesc Fabregas (16)kutoaka Bacrelona akikua
atauvaa moyo wa Arsenal moyoni mwake,akamsajili Robin Van Persie na Samir Nasri
akiamini hizzo zitakuwa silaha zake wakati akina Viera wakiondoka.
Lakini
alisahau kuwa mchezo wa soka ni kama mapenzi
unaweza ukamchagu mpenzi umtakae haijalishi kama unampenda au humpendi
siri inabali kuwa moyoni mwako,kama unataka pesa unamtafuta mpenzi mwenye pesa
ndivyo alivyofanya Nasri kwa kwenda Man City,kama unataka heshima na umaarufu
unamtafuta mpenzi mwenye heshima na maarufu kama alivyofanya Robin Van Persie
kwa kwenda Man U,kama unampenda mpenzi wako toka utotoni basi unamtafuta ndivyo
alivyofanya Cesc Fabregas kwa kwenda Barcelona.
Maisha ya
sasa yamezidi kubadilika na hata kwenda mbali zaidi na kusababisha wachezaji
kuhitaji mishahara mikubwa kutoka kwenye klabu yao baada ya kuyafikiria maisha
yao yatakuwae wakati watakapo stahafu soka,ndio maana Theo Walcot alikataa
kusaini mkataba mpya Arsenal mpaka alipoongezewa mshahara.Tusishangae nae
Welshere alifikia maamuzi kama hayo misimu miwili ijayo wakati mkataba wake
utakapokaribia kumalizika 2018.
Siamini kama
Wenger alishindwa umsajili Gonzalo Higuin,siamini pia kama alishinndwa
kumsajili Luis Gustavo ila tatitizo ni ugumu wa moyo wake kutotaka dunia ikimshuhudua
akifeli kaktika falsafa zake ndani ya Arsenal.Macho yake yanaamini mafanikio
yanaletwa na wachezaji kama Luis Suarez ama Robin Van Persie lakini hisia za
moyo wake zinaamini mafanikio yanapatikana kwa mtu kama usajili mpya Yaya Sanogo na Abu Diaby hapa ndipo
ninaposema Wenger mwenye moyo wa chuma unaofunikwa sura ya upole.
No comments:
Post a Comment