Amis Tambwe akishangilia goli |
STRAIKA Mrundi, Amisi Tambwe wa Simba amekuwa msumbufu kwa mabeki kwenye Ligi Kuu Bara huku akitesa kwa mabao saba, lakini benchi la ufundi la Yanga limemwangalia kwa umakini uchezaji wake na aina ya mabao anayofunga, kisha wakasema anakabika tu.
Benchi hilo likaenda mbali na kutamba kwa kusema kuwa hawana woga kabisa na Tambwe, labda angekuwa, Emmanuel Okwi raia wa Uganda kwa sababu ni mchezaji pekee wanayemhofia, ana mbinu nyingi, hatabiriki na ni msumbufu.
Hata hivyo, Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Burundi alifunga mabao 21 na sasa ndiye kinara wa mabao kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao saba amewaambia: “Thubutu yenu, lazima niwaumbue.”
Wachezaji wa Yanga pamoja na benchi lao la ufundi, wamekuwa wakifika kushuhudia mechi za Simba na hata walipoifunga JKT Ruvu Jumapili iliyopita, walikuwepo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Fred Minziro, ambaye ni Kocha Msaidizi wa Yanga alisema: “Tumemwona, Tambwe ni mchezaji mzuri ambaye sifa yake kuu ni hodari wa kufunga. Tambwe kama anapata pasi nzuri haoni kazi kufunga, anajua kucheza na ukimpa nafasi kidogo tu, umeumia.”
Minziro, ambaye kikosi chake hicho kitacheza na mahasimu wao, Simba Novemba 20 mwaka huu katika mechi ya Ligi Kuu aliongeza:
“Lakini pamoja na ubora wake, Tambwe anakabika kabisa. Hatuumizi kichwa kabisa kwenye kikosi chetu, kwa sababu tumeona ubora wake ana tageti nzuri ya kufunga na upungufu wake anakabika. Mtu ambaye anatuumiza kichwa na hata kama akirudi Simba leo atatupa presha ni Okwi tu.
“Okwi ni hatari na ana madhara makubwa kamwe huwezi kumfananisha na Tambwe hata kidogo. Nafasi zao ni tofauti na sifa zao ni tofauti lakini Okwi ni moto wa kuotea mbali,” alisema Minziro.
“Anajua kutafuta mpira kwa kukaba, ana kasi, chenga za maudhi na mbinu za kuwatoka mabeki wa timu pinzani na ukumbuke kuwa wakati wowote anaweza kusababisha tatizo langoni kwako.
“Lakini Tambwe yeye hayuko hivyo ukali wake ni kuziona nyavu tu, endapo utaziba njia unamaliza kila kitu,” alisema Minziro beki wa zamani wa Yanga huku akitambia safu yake ya ulinzi inayoongozwa na mabeki wa kati, Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kulia ni Mnyarwanda Mbuyu Twite na kushoto ni David Luhende.
Mabeki hao wamesema watamwonyesha kazi siku hiyo kauli iliyosisitizwa na Luhende aliyesema: “Hatishi sana ni kama washambuliaji wa timu nyingine, anakabika.”
Akizungumzia suala hilo, Tambwe alisema: “Najiamini na nitahakikisha nawafunga, tambo nyingi lakini mpira ni dakika 90 za uwanjani na hauchezwi nje ya uwanja
No comments:
Post a Comment