Prince Boateng |
Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Ghana, Kevin-Prince Boateng atakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya kujitafutia nafasi kwenye dimba la kombe la dunia dhidi ya Misri, kutokana na jeraha la goti.
Mechi hiyo itachezwa mjini Kumasi
Na baada ya kufanyiwa ukaguzi na madakatri, imegunduliwa kuwa Boateng lazima afanyiwe upasuaji kwenye goti lake la kushoto.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alipata jeraha hilo wakati wa mechi ya klabu yake ya Schalke ya Ujerumani kwenye mechi za ligi ya Bundesliga.
Kocha wa timu ya Black Stars, Kwesi Appiah, ameamua kutafuta mchezaji mwingine kuchukua nafasi ya Boateng.
Mechi za mkondo wa pili za kufuzu kwa kombe la dunia litakalochezwa nchini Brazil mwaka ujao, zitachezwa mjini Cairo, Misri tarehe 19 Novemba.
Hata hivyo, Ghana wameomba michuano hiyo kuhamishiwa kwingineko kwa sababu za usalama kufuatia hali ilivyo nchini Misri
No comments:
Post a Comment