Thursday, 10 October 2013

MCHEZAJI MAARUFU WA KRIKETI WA INDIA ASTAAFU

Tendulkar atacheza mechi yake ya mwisho mwezi ujao

Mchezaji maarufu wa Kriketi nchini India Sachin Tendulkar ametangaza atastaafu kutoka katika mchezo huo baada ya kucheza kwa mara ya 200 mwezi ujao.

Tendulkar mwenye umri wa miaka 40 na kinara wa zamani wa timu wa India , aliyestaafu kutoka kwa mchuano wa siku moja wa kimataifa mwaka 2012, atastaafu baada ya kucheza mechi mbili dhidi ya West Indies.
Tendulkar ndiye mchezaji aliyeweza kuwa na mikimbio mingi zaidi kuliko wote ikiwa 15,837 katika michuano 198 ya mataifa yenye hadhi ya juu au Tests na mikimbio mingine 18,426 katika michuano mingine 463 ya ODIs."ni vigumu kutafakari maisha bila kucheza Kriketi, kwa sababu ndio nimekuwa nikifanya tangu nikiwa miaka 11,'' alisema Tendulkar.
Alianza kucheza kimataifa akiwa na umri wa miaka16 mwezi Novemba mwaka 1989 na mwaka jana akawa mchezaji pekee katika historia ya mchezo huo kufikisha senchari 100.
"Maisha yangu yote nimekuwa nikiota kuhusu kucheza kriketi India. Na nimekuwa nikiishi katika ndoto hii kwa miaka 24 iliyopita,'' alisema.
Tendulkar alicheza mchezo wake wa mwisho wa michuano ishirini kati ya timu yake ya Mumbai na Rajasthan Royals inayoongozwa na skipa wa zamani wa India na mchezaji mwenzake Rahul Dravid.
Tendulkar atacheza katika mechi yake ya mwisho kitaifa nchini India na amesema kuwa litakuwa jambo la heshima sana kwake kuwakilisha nchi yake kote duniani.

No comments:

Post a Comment