Saturday, 5 April 2014

Kipre Tchetche atolewa Azam


STRAIKA wa Azam FC, Kipre Tchetche
ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha
timu hiyo kutokana na kuugua Malaria na upo
uwezekano wa kukosa mechi ya kesho Jumapili

dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja
wa Mabatini, Mlandizi Mkoani Pwani.
Pamoja na kukosekana kwa Tchethe kikosi
hicho kimeendelea kujifua kwenye uwanja wao
wa Azam Complex kwa ajili ya kusaka ushindi
zaidi na kinachofanyika sasa ni umakini kwa
kila mchezaji katika kufunga na kulinda lango
lao.
Tchetche ambaye anashika nafasi ya pili akiwa
na mabao 12 nyuma ya Mrundi Amissi Tambwe
akiongoza kwa kufunga mabao 19.
Straika huyo raia wa Ivory Coast, ameshindwa
kufanya mazoezi kwa siku mbili juzi Alhamisi
na jana Ijumaa hakuwepo kabisa baada ya
kuhudhuria matibabu hospitali.
Kocha msaidizi wa Azam FC, Mkenya Ibrahim
Shikanda alisema: “Tchetche ni mgonjwa
anasumbuliwa na Malaria na leo hayupo,
amekwenda hospitali kwa ajili ya matibabu
zaidi.”
Kocha mkuu wa kikosi hicho, Joseph Omog
alisema kumkosa Tchetche ni pengo lakini ana
imani atapata matibabu na kurejea uwanjani
mapema.
Katika hatua nyingine Azam inaendelea kujifua
kwa ajili ya mchezo huo na Mwanaspoti
limeshuhudia mazoezi yao ambapo suala la
umakini lilikuwa likisisitizwa zaidi.
Jopo la makocha la kikosi hicho, liliwagawa
wachezaji katika makundi mawili, wanaocheza
mbele walikuwa na Omog na msaidizi wake,
Kally Ongala wakati kundi la pili la walinzi,
lilikuwa na Shikanda.

No comments:

Post a Comment