Saturday, 5 April 2014

Torres asubiri chake Chelsea


LONDON, ENGLAND
CHELSEA italazimika kumlipa Fernando Torres
Pauni 10 milioni kama gharama ya mishahara
yake iliyobaki klabuni hapo baada ya kocha,

Jose Mourinho, kufichua wazi kwamba straika
huyo Mhispaniola hana chake tena Stamford
Bridge.
Mourinho amemponda staa huyo na kusema
sio straika baada ya kuboronga kwenye mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris
Saint-Germain Jumatano iliyopita.
Klabuni hapo, Torres analipwa Pauni 175,000
kwa wiki na kwenye mkataba wake amebakiza
miaka miwili.
Torres anafahamu wazi hakuna mahali kwingine
atakakoweza kulipwa kiasi hicho kwa wiki baada
ya kuondoka Chelsea hivyo atahitaji kulipwa
gharama zote za sehemu ya mkataba wake
uliobaki baada ya kutambua kwamba itakuwa
ngumu kuendelea kubaki klabuni hapo.
Mourinho anaamini kwamba Torres alichukizwa
na kitendo alichofanyiwa Mhispaniola
mwenzake, Juan Mata, ambaye kwa sasa
amehamia Manchester United na kushindwa
kujituma uwanjani. Torres na Mata walikuwa
marafiki wakubwa.
Torres ambaye alifunga mabao 23 msimu
uliopita na kutwaa ubingwa wa Europa League
chini ya kocha, Rafa Benitez, amefunga mara
mbili tu tangu Mata aondoke Stamford Bridge
Januari mwaka huu.
Hata hivyo, staa huyo wa zamani wa Liverpool,
hawezi kukubali kuondoka Chelsea hadi hatima
ya malipo ya mkataba wake itakapofikiwa.
Bilionea mmiliki wa Chelsea, Roman
Abramovich, alimnunua Torres kwa Pauni 50
milioni kutoka Liverpool ambako alikuwa
akilipwa Pauni 140,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment