Saturday, 1 March 2014

XAVI AKERWA NA UTARATIBU WA KOCHA BARCELONA


BARCELONA, HISPANIA
KIUNGO, Xavi, amekiri kukerwa na mtindo wa
kocha mpya wa Barcelona, Gerardo Martino,
kutokana na kumpunguzia muda wa kucheza
kwenye mechi.

Staa huyo Mhispaniola alibainisha wazi
kuchukia jambo hilo licha ya kudai kwamba
hawezi kusababisha matatizo yoyote kutokana
na hilo.
Xavi, mwenye umri wa miaka 34 amecheza kwa
dakika 90 mechi tisa tu kati ya 25 za Ligi Kuu
Hispania msimu huu na kwamba jambo hilo
limemweka kwenye wakati mgumu.
“Inanichanganya ninaposhindwa kupata nafasi
ya kutosha uwanjani, lakini siku zote
naheshimu uamuzi wa kocha,” alisema kiungo
huyo.
“Ni kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.
Nimejifunza vya kutosha kwamba sipaswi
kuingilia kati uamuzi wa kocha. Hapa
Barcelona, sote tunafahamu hakuna mkubwa
zaidi ya kocha.”

No comments:

Post a Comment