Saturday, 1 March 2014

AIBU: Mke wa zamani adai Eto’o ana miaka 39


LONDON, ENGLAND
KOCHA, Claude Le Roy, amesema alizungumza
na Samuel Eto’o kwenye simu na kwamba
alikasirika sana kwa kitendo cha umri wake
kuhojiwa.

Kocha wa sasa anayemnoa straika huyo wa
Cameroon kwenye klabu ya Chelsea, Jose
Mourinho, kwenye mazungumzo yake ya
kawaida tu na tajiri mtengeneza saa wa Uswisi
ambayo yalinaswa kwa siri na kurekodiwa,
alisema hafahamu umri halisi wa Eto’o kama ni
miaka 32 kama ilivyo kwenye pasipoti yake ya
kusafiria au ni miaka 35.
Kabla ya kufikia kwenye kuhoji umri wa Eto’o,
Mreno Mourinho alikuwa akijadili uwezo wa
mastraika wake kwenye klabu ya Chelsea na
mustakabali wa kunyakua ubingwa msimu huu.
Mourinho alilalamika kwamba washambuliaji
wake wote wanamwangusha kutokana na
kushindwa kufunga mabao. Washambuliaji
waliopo kweye kikosi cha Chelsea wote ni
makini; Demba Ba, Fernando Torres na Eto’o,
lakini wote hao wamekuwa butu na kushindwa
kufunga mabao.
“Tatizo la Chelsea hakuna wafungaji,” alisema
Mourinho. “Ninaye Eto’o, lakini umri wake ni
miaka 32, pengine inaweza kuwa 35, huwezi
kujua,” alisema Mourinho.
Kocha, Le Roy, aliyewahi kumnoa Eto’o kwenye
kikosi cha Cameroon, anasema straika huyo
hakupendezwa na kauli ya Mourinho kumsema
kwamba umri wake ni mkubwa kuliko
unaotambulika rasmi.
Eto’o amesisitiza kwamba umri wake ni miaka
32. Jumatano iliyopita, Chelsea ilikuwa na
mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
dhidi ya Galatasaray na kwamba iliaminika
kwamba baada ya mchezo huo, Mourinho na
Eto’o watahitaji kuwekana sawa.
Lakini, wakati Eto’o akisisitiza kwamba umri
wake ni miaka 32, kama ulivyoandikwa kwenye
pasipoti yake, mke wa zamani wa staa huyo
ameibuka na kuchafua zaidi hali ya hewa baada
ya kueleza kwamba umri wa supastaa huyo wa
zamani wa Barcelona ni mkubwa kuliko hata
uliotajwa na Mourinho.
Mkewe afichua
Mrembo, Anna Barranca, ambaye alizaa na
Eto’o mtoto mmoja, amefichua wazi na kusema
umri wa staa huyo ni miaka 39.
Mourinho alihisi Eto’o anaweza kuwa na umri
wa miaka 35, lakini mwanamke huyo wa
Kitaliano ametoa kali baada ya kudai kwamba
Eto’o amepunguza miaka saba ya umri wake wa
kweli.

No comments:

Post a Comment