Monday, 24 March 2014

RVP azua hofu, apelekwa Uholanzi


STRAIKA, Robin van Persie, amepandishwa ndege hadi kwao Uholanzi ili akakutane na daktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya  kumfanyia matibabu ya haraka yatakayomfanya apone kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil baadaye mwaka huu.
Staa huyo wa Manchester United, aliumizwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiakos Jumatano iliyopita na alionekana akitembea kwa msaada wa magongo akiwa hospitali ya Erasmus ya mjini Rotterdam, Uholanzi.
Straika huyo wa Uholanzi anatibiwa na daktari bingwa wa upasuaji, Rien Heijboer. Ripoti za awali zinadai kwamba kuna hofu kubwa kwamba mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita na hilo ni pigo kubwa kwa Man United inayojaribu kuweka mambo sawa kwenye Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Daktari huyo aliwahi kumtibu Van Persie kipindi alichokuwa kwenye kikosi cha Arsenal. Heijboer pia aliwahi kumsaidia Zlatan Ibrahimovich kupona matatizo ya goti.

No comments:

Post a Comment