Wednesday, 5 February 2014

MREMBO AMZIMIA GERALD


MWIGIZAJI wa kike anayeng’ara kwenye sinema
ya Sex And The City, Kim Cattrall, amefichua
kwamba amekuwa akiwaonea wivu watu
wanaopata fursa ya japo kumgusa tu kiungo wa
Liverpool, Steven Gerrard.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 57
ambaye anatumia jina la Samantha Jones
kwenye mfululizo wa sinema hizo, ni shabiki wa
Liverpool na mara kadhaa ameonekana
uwanjani Anfield kwenye mechi za soka.
Mrembo Kim aliyezaliwa kwenye jijini Liverpool
alihama na wazazi wake akiwa na umri wa
miaka mitatu tu wakati wazazi wake
walipohamia Canada mwaka 1956.
Katika kubainisha mapenzi yake kwa staa huyo
wa England, Kim alituma ujumbe kwenye
Twitter pamoja na picha inayomwonyesha
Gerrard akiwa ameshikwa mgongoni na kocha
wa viungo, aliandika: “Najisikia wivu sana.
Nilikutana na Steven mara chache lakini
sitapata nafasi hata ya kumkaribia tu.”

No comments:

Post a Comment