Wednesday, 5 February 2014

WENGER;NILIJUA NASAJILI MGONJWA


ENE Wenger ametoa kali ya mwaka baada ya
kudai kwamba alifahamu mchezaji mpya
waliyemsajili mwezi Januari, Kim Kallstrom ni
mgonjwa na kwamba kwake si kitu muhimu
sana hata kama atashindwa kucheza mechi
yoyote Arsenal.

Mchezaji huyo aligundulika kuvunjika mfupa
wa mgongo, lakini kwa presha ya siku ya
mwisho ya kufunga usajili, Wenger aliamua
kufanya usajili wa kiungo huyo licha ya
kwamba madaktari walimwambia kuwa ni
mgonjwa.
Madaktari wa Arsenal waliompima staa huyo
walimpa taarifa Wenger kwamba staa huyo
amevunjika moja ya mifupa mgongoni wakati
walipomfanyia uchunguzi huo Ijumaa iliyopita.
Lakini, Wenger aliyepitisha usajili wake na juzi
Jumapili alikiri kwamba ameamua kumnasa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na
atakuwa kikosini kwake hata kama hatacheza
mechi yoyote Arsenal hadi mwisho wa msimu.
Kallstrom atakakuwa nje ya uwanja kwa kipindi
ambacho kinatajwa kuwa ni wiki sita, klabu
yake ya zamani ya Spartak Moscow ndiyo
itakayokuwa ikimlipa mshahara na baada ya
hapo litakuwa jukumu la Arsenal.
Wenger alisema: “Nina hakika kama umewahi
kucheza mpira, lazima uliwahi kucheza huku
sehemu moja ya mfupa ikiwa imevunjika
kidogo. Huwezi kujijua. Mimi nililiwaza hilo
lakini nilifikiria zaidi kumaliza dili. Hawa
Spartak watamlipa mshahara wake kwa wiki
sita, lakini matarajio yangu atakuwa nje kwa
wiki nne hadi sita. Acha hili lipite tutajua
mwisho wa msimu kama tulikuwa sahihi au
tulikosea.”

No comments:

Post a Comment