Thursday, 13 February 2014

BALOTEl AELEZA ALICHOKIMIC WINGEREZA


MILAN, ITALIA
SUPASTAA, Mario Balotelli, Jumamosi iliyopita
alimwaga chozi wakati klabu yake ya AC Milan
ilipochapwa 3-1 na Napoli kwenye Serie A,

lakini alipoulizwa mwenyewe alijibu
amewakumbuka sana mashabiki wake
Manchester City.
Machozi ya staa huyo aliyoyatiririsha akiwa
kwenye benchi, yaliibua mjadala huku mdogo
wake, Enock Baruwah, akidai ilikuwa furaha ya
Balotelli kutambua kwamba ni baba wa mtoto
Pia, ambaye awali alimkana wakati mrembo
Raffaella Fico alipokuwa mjamzito.
Vipimo vya vinasaba vya damu vimeonyesha
kwamba straika huyo ndiye baba wa mtoto wa
mrembo huyo wa Kitaliano.
“Nimewamisi mashabiki,” alisema Balotelli
alipohojiwa na Jarida la FourFourTwo.
“Nitawaambia vitu ambavyo sijavimisi. Sijui
vyakula, hali ya hewa na mambo mengine,
nilichokimisi ni mashabiki wa Manchester City.
Nawakumbuka sana licha ya kwamba mashabiki
wa Milan wapo vizuri.”
Balotelli alijiunga na AC Milan Januari mwaka
jana akitokea Manchester City ya England.

No comments:

Post a Comment