Thursday, 13 February 2014

YANGA WAACHA KASEJA NA OKWI SAFARI YA MOROCCO


JESHI la wachezaji 19 la kikosi cha Yanga
linaondoka leo Alhamisi alfajiri kuifuata
Komorozine ya Comoro, lakini kocha mkuu wa
timu hiyo, Hans Van Pluijm amewatema nyota
kumi kwenye msafara wake wakiwamo kipa

Juma Kaseja na mshambuliaji, Emmanuel Okwi.
Yanga inakwenda kurudiana na Wacomoro hao
katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Awali
Yanga ilishinda nyumbani mabao 7-0.
Kocha huyo alisema Kaseja aliyedaka kwenye
mechi iliyopita, ameachwa kutokana na
matatizo ya kiafya na Okwi ni kutokana na
utata wa usajili wake.
“Bado tunataka ushindi, ukiangalia wachezaji
ambao tunaondoka nao ni wale waliokuwa
sawa katika mazoezi yetu ya wiki hii, hatutaki
kwenda kujilinda sababu ya ushindi wetu wa
mchezo wa kwanza,” alisema.
“Kuna uwezekano wa kikosi kitakachoshuka
uwanjani siku ya Jumamosi kuwa na mabadiliko
kidogo, lakini kwa sasa siwezi kukueleza nani
na nani wataingia au kutoka, uamuzi wa
mwisho tutafanya siku moja kabla ya mchezo.”
Licha ya Kaseja na Okwi, nyota wengine
walioachwa ni viungo Nizar Khalfan, Salum
Telela ambao ni wagonjwa kama ilivyo kwa
washambuliaji Jerry Tegete, Reliants Lusajo,
Shaaban Kondo na Hussein Javu pamoja na
Bakari Masoud na beki Ibrahim Job.
Walioondoka ni makipa Deogratias Munishi
‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’, Mabeki ni
Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na
Rajab Zahir.
Viungo ni Athuman Idd ‘Chuji’, Frank Domayo,
Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Mrisho
Ngassa, Simon Msuva, Hamis Thabitna David
Luhende wakati washambuliaji ni Hamis Kiiza,
Said Bahanuzi na Didier Kavumbagu.

No comments:

Post a Comment