Friday, 31 January 2014

SIMBA YAMREJESHA OEINO KUNDINI


KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amemsamehe beki wake wa kati, Joseph Owino
na kumrejesha kwenye kikosi kinachojiandaa na
mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Oljoro

Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Beki huyo raia wa Uganda alikuwapo kwenye
mazoezi ya jana Jumatano jioni kwenye Uwanja
wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Owino alitimuliwa na kocha wake katika
mazoezi wiki iliyopita yaliyofanyika kwenye
uwanja huo chakavu ulioko Shekilango.
Beki huyo wa Uganda alidaiwa kujibizana na
bosi huyo kutokana na kukasirishwa na lugha
mbaya ya Mcroatia huyo ingawa baadaye kocha
huyo alimruka na kudai kwamba alikuwa
hafuati maelekezo yake.
Owino alionekana katika mazoezi ya timu hiyo
jana Jumatano jioni chini ya Logarusic
anayesaidiana na Selemani Matola.
Kabla ya kuanza mazoezi alimuomba msamaha
kocha na wachezaji wenzake pamoja na benchi
zima la ufundi kutokana na kitendo chake cha
utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa taarifa ilizozipata Mwanaspoti,
beki huyo juzi Jumanne alimuandikia barua
kocha wake ya kumuomba msamaha
iliyopelekwa na meneja wa timu hiyo, Nico
Nyagawa lakini Kocha aliigomea kwa madai
kwamba alitaka mchezaji aipeleke mwenyewe.
Baada ya Owino kuipeleka barua hiyo, kocha
alimtaka aombe radhi kwa wachezaji wenzake
jambo ambalo alilifanya na kusamehewa.
Logarusic alisema kuwa suala limemalizika na
sasa hakuna tatizo tena katika timu na
wanasonga mbele.

No comments:

Post a Comment