Friday, 31 January 2014

ROONEY KUBAKI MAN U


MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne
Rooney amekubali kusaini mkataba mpya
utakaomweka Old Trafford zaidi ya mwaka
2015 huku akiwa mchezaji anayelipwa zaidi
klabuni hapo.

Rooney amesuasua kusaini mkataba mpya Old
Trafford na ilidaiwa kwamba alikuwa
anajiandaa kuondoka mwishoni mwa msimu
kwa ajili ya kupata changamoto mpya ya soka
nje ya Man United.
Mkataba wa Rooney unatarajiwa kumalizika
mwishoni mwa msimu ujao Juni 2015 na
kulikuwa na wasiwasi kwamba staa huyo wa
zamani wa Everton alikuwa anataka kuondoka
bure mwishoni mwa msimu ujao hili apate
fedha nyingi zaidi.
Hata hivyo, kocha David Moyes amefanikiwa
kumshawishi nyota huyo kubaki lakini kwa
gharama za kumlipa mshahara wa Pauni
300,000 (Sh.750 milioni) kwa wiki ambao
unaweza kuwa wa mwisho kwake klabuni hapo.
Wakati huohuo, licha kumnasa kiungo
mchezeshaji wa Chelsea, Juan Mata na
kufanikiwa kumbakiza Rooney, Moyes
amekumbana na pigo baada ya kiungo wa
Juventus aliyekuwa anamwinda, Arturo Vidal
kusisitiza kwamba atabaki klabuni hapo.
Moyes ameshasafiri mpaka Italia kwa ajili ya
kumwangalia nyota huyo wa kimataifa wa Chile
ambaye yupo katika kiwango cha juu na
alikuwa anataka kumchukua katika kikosi chake
kwa ajili ya kukitia makali na kukirudisha katika
ushindani.
Moyes atalazimika kuongeza juhudi zake kwa
kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ambaye
anaweza kuuzwa.

No comments:

Post a Comment