Friday, 31 January 2014
Ligi Kuu yatumia mabilioni usajili 2013
KLABU za Ligi Kuu England zimetumia Pauni
660 milioni kwenye uhamisho wa wachezaji wa
kimataifa kwa mwaka jana pekee, huku zaidi ya
pauni 50 milioni zikitumika kwenye ada za
kulipwa mawakala, imeripoti Fifa.
Klabu za Italia zinafuatia kwa kushika namba
mbili kwa kutumia pesa nyingi baada ya
kuponda pauni 286 milioni, kisha inakuja
Ufaransa (pauni 253milioni), Hispania (pauni
192 milioni) na Ujerumani (pauni 144 milioni).
Nchi ya Brazil imeongoza kuwa na wachezaji
wengi waliouzwa ng’ambo, ambapo jumla ni
wachezaji 1,558 sawa na asilimia 13.
Klabu za Hispania zimeingiza pesa nyingi zaidi
kwenye usajili huo kwa mwaka jana baada ya
kuvuna pauni 150 milioni kutokana na kuuza
wachezaji wake ng’ambo.
“Kuna klabu chache sana zilizofanya usajili
mkubwa ambao ulitetemesha sokoni, lakini
usajili mwingine ulikuwa wa kawaida tu,’
alisema Mark Goddard, meneja wa masuala ya
uhamisho wa wachezaji Fifa.Kwa England usajili
mkubwa wa mchezaji aliyehamia kwenye Ligi
Kuu ni ule wa Arsenal walipomnasa Mjerumani
Mesut Ozil kwa pauni 42.4 milioni kutoka Real
Madrid, wakati uhamisho wa kuuza nje ya nchi
ni ule wa Gareth Bale kutoka Tottenham
kwenda Madrid kwa pauni 85.3 milioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment