Friday, 31 January 2014

BONGO MOVIE YAPATA UONGOZI MPYA


MAPEMA mwezi huu, Chama cha Filamu
Tanzania kilipata uongozi mpya, Steven
Mengele maarufu Steve Nyerere alichaguliwa
kuwa mwenyekiti akirithi mikoba ya Vicent
Kigosi ‘Ray’ aliyemaliza muda wake
.
Wengine waliopata nyadhifa za juu katika
uongozi huo ni Makamu Mwenyekiti Mahsein
Awadh ‘Dokta Cheni’, Katibu Mkuu William
Mtitu na naibu wake, Devotha Mbaga huku Issa
Mussa ‘Cloud’ akichaguliwa kuwa Mweka
Hazina.
Kama ilivyo sehemu yoyote duniani uongozi
mpya unapoingia madarakani, huweka malengo
na vipaumbele vyake ili kuwawakilisha vyema
wale waliowachagua.
Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti,
Steve Nyerere alizungumzia mikakati yao
mitano muhimu wanayotaka kuipa kipaumbele
kuwa ni;
Kudhibiti wizi wa kazi za filamu
Suala kubwa ambalo limekuwa likiwaumiza
wasanii ni wizi wa filamu, hasa unaofanywa na
wachuuzi wenye vibanda vya kuuza na
kutengeneza santuli ‘CD’. “Tumekosa utaratibu
maalumu wa kudhibiti wizi wa kazi zetu, watu
wamejifungulia vibanda wanatengeneza santuli
za filamu zetu na kuziuza kwa bei chee bila
ridhaa yetu.”
“Hili linatuumiza sana wasanii, hivyo uongozi
wetu umepanga kushirikiana na serikali ili
kudhibiti suala hilo, hatutakaa chini kamwe
tukiendelea kushuhudia uhalifu huu mkubwa
wa kazi zetu,” anasema Nyerere ambaye ni
mwigizaji wa filamu za vichekesho maarufu
komedi.
Mavazi na nidhamu
“Imekuwa ni aibu sasa, wasanii wanavaa mavazi
ya ajabu na udhalilishaji hadi watazamaji
wanaona aibu kutazama filamu zetu. Uongozi
mpya kwa kushirikiana na wadau muhimu
tumepanga kupambana na kadhia hii ili
kurejesha heshima ya Bongo Movie.”
“Tunataka mtu avae kutokana na uhusika wa
sehemu anayocheza, kama ni mama wa
nyumbani avae kama mama wa nyumbani na
kama ni changudoa avae kama changudo si
filamu nzima wote wamevaa kama
machangudoa,” anasema.
Ubora wa filamu
Nyerere anasema suala la ubora mdogo wa
filamu za Bongo si jambo geni, filamu za
Bongo zimekuwa zikifyatuliwa kama njugu, kila
siku kuna filamu mpya jambo ambalo amedai
hawezi kulifumbia macho.

No comments:

Post a Comment