Kocha wa Azam, Stewart Hall. |
LIGI Kuu Bara ina wazungu wawili tu. Sikia walichosema. Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts amesema Azam FC ndiyo timu inayomfuata kwa ubora kwa sababu ndiyo inayocheza mpira mzuri na ilimpa ushindani kwenye mzunguko wa kwanza unaomalizika Alhamisi wiki hii.
Mwingereza wa Azam, Stewart Hall naye amekiri kuwa
baada ya klabu yake kwa ubora, ya pili inayomfuatia ni Yanga ya Brandts
wala si Simba au Coastal Union.
Azam ndiyo inayoongoza kwa pointi 26 sawa na Mbeya
City inayoshika nafasi ya pili lakini wanatofautiana idadi ya mabao,
Yanga ni ya tatu ina pointi 25 wakati Simba ni ya nne ina pointi 21.
Timu hizo zote zimebakiza mechi moja za kumaliza
mzunguko huo na Yanga ilianza kumfunga Azam kwenye mechi ya Ngao ya
Hisani na Azam ililipiza kisasi kwa kuifunga Yanga 3-2 katika mechi ya
ligi.
Akizungumza na Mwanaspoti,
Brandts alisema: “Timu yangu ni bora na Azam inafuata. Azam inacheza
vizuri na uliona walitufunga, huwezi kufananisha Azam na timu nyingine
kwa ubora.”
Naye, Stewart alisema: “Ligi imekuwa ngumu msimu
huu na kila timu ni nzuri na ndiyo maana hata matokeo mengi ni ya sare.
Unapozungumzia ubora ya kwanza ni yangu na Yanga ndiyo inayofuata. Yanga
wako vizuri msimu huu, wana wachezaji wazuri na wazoefu waliokaa pamoja
muda mrefu.”
“Huwezi kuifananisha Yanga na timu nyingine kwenye
ligi hii ukitoa yangu ya Azam, si Simba au nyingine yoyote, kidogo
Mbeya City wanakuja vizuri,”alisema Stewart.
Azam itamaliza mechi yake ya mwisho na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment