MASHABIKI wa Mbeya wamekerwa na kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Sokoine na sasa wanataka kushinikiza wakabidhiwe majukumu na uongozi ili kuepuka fedheha.
Lakini Kocha Msaidizi wa Prisons, Oswald Morris
amesema hajui tatizo liko wapi kwa timu yake kwani wachezaji wanajituma
lakini mwisho wa siku wanaambulia matokeo mabovu ambayo yamezidi
kuwakera
mashabiki wa Mbeya.
mashabiki wa Mbeya.
Prisons inakamata nafasi ya 13 kati ya timu 14
zinazoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo 12, imeshinda
mmoja, imetoka sare tano, imefungwa michezo sita na ina pointi nane.
Morris ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo zamani
alisema muda mwingine machozi yanamtoka kwa matokeo wanayoyapata na
kuwataka wadau kuwasaidia kujua tatizo la timu yao liko wapi.
“ Inaumiza sana, sijui tatizo liko wapi, timu
inacheza katika kiwango cha juu lakini matokeo yanatuhukumu, wachezaji
wanapigana mpaka mwisho lakini ndio hivyo, muda mwingine natokwa na
machozi kwani sielewi tatizo, naona timu inapotea wakati soka lipo,
labda wadau watusaidie kama wameona tatizo ndani ya timu hii ili
lirekebishwe na timu irudi katika hali yake,” alisema Morris.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi, Prisons
ilipukutisha mastaa wote wa timu hiyo na kusajili wachezaji wengi
chipukizi na baadhi ya mastaa hao waliitabiria timu hiyo kutofika mbali
kwa madai waliachwa kwa fitna wakati bado walikuwa na uwezo wa kuibeba
timu hiyo.
Timu hiyo imebakiwa na mechi dhidi ya Rhino Rangers ugenini kabla ya ngwe ya kwanza ya ligi kumalizika.
No comments:
Post a Comment