Wakimbiaji 17 wamesimamishwa kukimbia kutokana na madai ya kutumia dawa za kusisimua misuli |
Kenya imekosolewa na Shirika la kudhibiti matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa kukosa kufanya uchunguzi katika ongezeko la visa vya wakimbiaji wa Kenya wanaoshukiwa kutumia dawa hizo.
Tangu mwaka wa 2012 wakimbiaji 17 wamesimamishwa kwa muda kutoshiriki mashindano ya kimataifa kwa madai ya utumizi wa dawa hizo za kusisimua misuli, ikilinganishwa na 2 tu kati ya mwaka wa 2010 na 2011.
Shutma hizi zitazungumziwa katika kongamano la shirikisho la kukabiliana na matumizi ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli katika michezo huko Johannesburg mwezi ujao
Ingawa shirika hilo halina uwezo wowote wa kuiwekea Kenya vikwazo, linaweza kuamua kuwa Kenya haifuati Sheria iliowekwa.
Hata hivyo ni jukumu la barala la kimataifa la michezo ya Olimpiki kuamua ikiwa wachezaji wanaweza kusimamishwa kukimbia siku zijazo.
"Ikilinganishwa na nchi zingine, tatizo la Kenya si kubwa zaidi" asema mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya, Isaiah Kiplagat.
Vikwazo hizo zinaonekana kutotekelezwa kwa sasa, lakini mkurugenzi wa shirikisho la kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli David Howman ameuudhika kwa sababu Kenya haijachukua hatua zozotete tangu madai hayo kutolewa.
David anatarajiwa kutaja Kenya kama nchi ngumu kushirikiana na shirikisho lake katika kongamano hilo huko Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya Isaiah Kiplagat na wizara ya michezo, shirikisho la kukabiliana na matumizi ya dawa ya kusisimua misuli iliwapa fursa hadi Novemba mwaka huu kutoa ripoti kuhusu hatua walizochukua lakini BBC imebaini kuwa, chini ya wiki mbili kabla ya kongamano hilo, hamna habari zozote kutoka kwa chama cha wanariadha cha Kenya.
Imebainika kuwa baraza lililoundwa na mashirika ya michezo ili kuangazia madai hayo kwa haraka, halijawahi kufanya mkutano tangu kuundwa mwaka uliopita.
Rodney Swigelaar mkerugenzi wa shirikisho la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli barani Afrika alisema:
"Tumekufa moyo, ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu twende huko na hata zaidi tangu uvumi wa madai hayo kuanza.
"hatua yao ya kuakhirisha uchunguzi imetuudhi,siwezi kusema rasmi wamefikisha wapi upelezi wao.
"Tumekua watulivu sana, wakati mambo haya yanafanyika mahali popote, ni jukumu letu kwenda kule na kuuliza ni nini chanzo chake na ni kwanini watu hawafuati sheria"
Lakini Kiplagat ameiambia BBC "naweza kudhibitishia kila mmoja kuwa baraza lililobuniwa na serikali itaanza kazi yake hivi karibuni.
Tunatumaiupelezi huo utaanza kabla ya kongamano la shirikisho la (WADA) kuanza. Sidhani matumizi ya dawa hizo ni tatizo kubwa sana Kenya. Wanariadha wetu wakuu walipimwa kabla ya kuenda London na pia kabla ya mashindano ya kimataifa ya IAAF huko Moscow mwaka huu.
Hata hivyo WADA inaweza kubuni kamati huru nchini Kenya kama ilivyofanya Jamaica licha ya uhakikisho wa Kiplagat
No comments:
Post a Comment