.
Agust 28
-2013 mwanaharakati wa haki za kibinadamu Matin Luther King Jr,alikamilisha
miakahamsini tangu atoe hotuba yake ya ‘I have a Dream’
Kwa wakati
huo Martin Luther akitoa hotuba hio mbele ya umati wa wamarekani,watu wengi
waliona kama ni ndoto tena isiokuwa ya kwel,katika hotuba yake alieleza ni kwa
jinsi gani ana ndoto siku moja mtu mweupe na mtu mweusi watakuwa na haki sawa
duniani kila mmoja atamwona mwingine ana dhamani.
Yalikuwa ni
maneno yaliougusa hisia za mtu mweusi na mtu mweupe,mtu mweusi alitamani ndoto
hiyo itokee na kuwa kweli ili mateso wanayoyapata kutoka kwa mtu mweupe yawe na
kikomo,mtu mweupe alitamani ndoto hiyo ibaki kuwa na ndoto na isiwe kweli ili
azidi kumnyonya mtu mweusi na kumwongoza wakati wote wa maisha yake.
Miaka 50
imeshapita tangu hotuba hii itoke kwa sasa sio ndoto tena,yaliyotabiriwa mengi
yameshatokea.Taifa kubwa kama Marekani linaongoza na mtu mweusi Barak
Obama,inchi kama Ujerumani ilikuwa inawabagua hadi wazungu wenzake kama sio
mzaliwa wa taifa hilo leo inaamtegemea beki mweusi Jerome Boateng,falsafa za
waitaliano zimebadilika kutoka kuwachukia watu weusi mpaka kumpenda Mario
Baloteli.
Akili za
Martin Luther zilitaka dunia iongozwe na watu wenye uwezo wa kuongoza wala sio
kigezo cha rangi ya mtu,kama leo angekuja dunia angefurahi kama angekwenda
inchi za mwenzetu zilizoamua kuwapa madaraka watu weusi kwa ajl ya uwezo wa
kuongoza,lakini atahuzunika kama kija katika soka la Tanzania na kuangalia akili
za viongozi wa soka wakiwa na ndot za kushiriki kombe la dunia lakini mioyo yao
ikijua hilo haiwezekani.
Siku zote
mtu hawezi kuudanganya moyo wake,si kweli kwamba vipaji vilivyopo Tanzania haviwezi kuipeleka Taifa Stars Qatar
2022 bali ni utawala wa soka mbovu wa soka unaoamini kwa kuungaunga timu
tunaweza tukapata timu bora ya kwenda kucheza fainal za kombe la dunia huku
ndani ya mioyo yao ipo saauti inayobishana nao ikiwaambi mpira unahitaji
maandalizi ya kweli.
Kilio cha
hotuba ya ‘I have a Dream’ kilikuwa ni kuleta mabadiliko sio ya rangi tu bali
hata kwa watu wenye uwezo wa kufanya jambo Fulani wapewe nafasi,haki iwe sawa
kwa wote bila kuangalia huyu ni nani,kama haki ya mtu ni kuoongoza na wwew
unamnyima inamaana unamnyima yake yake anayostahili na kama mtu hastahili
kuongoza alafu wewe unampa nafasi hiyo inamaana umepa mtu haki asiyostahili.
Katika
utawala wa soka la Tanzania ukiongozwa na shirikisho la mpira wa miguu(TFF)wapo
watu weenie ndoto za Martin Luther kwenye mawazo ya akili zaolakini kwenye
mioyo yao hilo haliwezeani unajua ni kwa nini?Uchaguzi unaokuja wa TFF umetupa
picha halisi,kama mgombea amabae watanzania wanamwamini anaweza kuleta
mabadiliko ya soka hapa inchini lakini walioshikilia mpini wanamwondoa kwa
sababu zisizofikirika kwa akili ya kawaida.
Viongozi
hawa wanatumia muda mwingi kufikiria mpira ni kama majira ya mwaka yanabadilika
kuendana na wakati,hapa ndipo wakatuletea kamati ya ushindi ya Taifa
Stars,sipati picha kama Shirikisho la mpira la Ujeremani wangeunda kamati ya
kisiasa ya ushindi siamini kama leo tungewaona akina Ozil,Gotze,Muller na
wengine.Sipati picha kama Spain wangewatengezea kamati akina Xavi na Iniesta.
Klabu zetu
za ligi zinatua jina la kitabu linalosadiki kilichopo ndani ya timu ya
Taifa,haiwezekani klabu ziwe katika viwango vya chini kasha timu ya taifa iwe
ya kushiriki kombe la dunia,Klabu hazituneshi rangi ya kijani na matumaini
katika siku za usoni,leo hii wachezaji kama Mbwana Samatha na Tomas Ulimwengu
ni maarufu baarani Afrika kuliko klabu zetu za Tanzania hii ni kwa sababu
wanacheza kwenye klabu eynye maleng ya siku moja kuwa moja ya klabu bora
duniani TP Mazembe.
Mpira wetu
umebaki kwenye ndoto zisizotokea,fitina na siasa zinafanya mambo magumu kuwa
marahisi na marahisi kuw magumu,Ujerumani ilianzisha mfumo wa kukuza vipaji
katika academy a soka ndio maana leo wana kundi kubw ala wachezaji akina Tom
Kroos,Tomas Muller,Mari Gotze,Mesut ozil na wengine wengi bao wanamiaka ya
kuendelea kutetemesha ardhi ya mashindno ya kombe la dunia hata kama akina Lahm
na wangongwe wengine wataondoka haya ni mandalizi ya muda mrefu ya yanaipa
matunda soka ya Uerumani kuanzia ngazi za klabu mpaka timu ya Taifa.
Soka la
Tanzania limebakia kwenye hotuba ya martin Luther King Jr na ‘I have a Dream’bado
watanzania wamejawa na ndoto za kuiona timu ya ya taifa ikishiriki kombe la
dunia lakini hili haliwezekani kiuhalisia kama utawala wa soka hautabadilika na
kuwa na haki sawa kwa mtu mwnye uwezo wa kuongoza.
No comments:
Post a Comment