Friday, 18 October 2013

AL AHLY KUINGIA IWANJANI NA MATATIZO


Al Ahly inaingia katika mechi ya mkondo wa pili wa michuano Klabu Bingwa barani Afrika dhidi Coton Sport mwishoni mwa wiki huku ikikabiliwa na matatizo lukuki.
Timu hiyo sasa itabidi kuwa na wachezaji wake maarufu ambao wamekata tamaa, kutimuliwa kwa kocha na kuchezea katika uwanja usio na mashabiki.
Jambo linaonekana kama ni matukio ya kawaida kwa timu hiyo yenye rekodi ya kunyakua ubingwa wa Afrika mara saba baada ya kutoka sare ya 1 -1 nchini Cameroon wiki mbili zilizopita imekuwa katika hali isiyo ya kuridhisha wiki hii.
Ahly imetoa wachezaji nane wanaochezea timu ya Taifa ya Misri iliyokubali kipigo cha mabao 6 -1 kutoka kwa Ghana katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kucheza kombe la dunia iliyopigwa siku ya jumanne, na kuondoa matumaini ya Misri kwenda kucheza fainali hizo nchini Brazil mwaka 2014.
Baada ya kuona ndoto ya kucheza kombe la dunia imefifia mchezaji mkongwe anacheza nafasi ya kiungo Mohamed Aboutrika amesema atastaafu soka baada ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika kumalizika.

No comments:

Post a Comment