Roben |
Mholanzi huyo alifungia The Bararian goli la tatu baada ya Frank Ribery na Tomas Muller kuifungia Bayern magoli ya kuongoza katika mchezo huo.
"Sikutegemea kama mchezo ungekuwa mrahisi kiasi kile Roben aliuambia mtandao wa skysport.
"Hii ni tikect kubwa sana kwetu,kwa kweli nilitegemea upinzani mkubwa kutoka kwa City.
"Walitupa nafasi kubwa na sisi tulitumia nafasi hizo vizuri zaidi,tuna washambuliaji wenye uwezo mkubwa na ndio maana kulikuwa na tofauti kati ya wao na sisi.
"Kadi nyekundu kwa Jerome Boateng haikutufurahisha lakini tulikubaliana na hali tukaendeleza mashambulizi na timu ikabaki katika kiwango bora
"Watu wanatufananisha sisi na Barcelona,sisi tutabaki kuwa Bayern Munich,Roben aliongeza,tunawachezaji wazuri,wanazidi kuongeza ukubwa wa kikosi.
"Msimu uliopita tulikuwa tumeimarika lakini msimu huu tumeimarika zaidi kutokana na uwezo wa kocha wetu.Akizungumzia uwezo wa Guardiola,,Roben alisema
"Guardiola anapumua na kufikiria soka mda wote, kila wakati anazungumzia mpira wa miguu,umri wangu unazidi kusogea lakini nitazidi kujifunza mambo mengi kutoka kwake,nina mwelewa vizuri sana haijalishi nina umri(29)jambo la msingi yeye ni kocha muhimu kwangu"
No comments:
Post a Comment