Haruna Niyonzima akiwa amekaa nyumbani kwake Magomeni baada ya kumaliza kuzima shoti ya umeme iliyokuwa inateketeza mali zake |
Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima ambaye pia ni mchezaji wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom wa timu ya Young Africans amepatwa na jangwa la kuunguliwa kwa baadhi ya mali zake kufuatia kutokea shoti ya umeme leo asubuhi.
Niyonzima ambaye anaishi eneo la Magomeni Makuti amekutwa na na tatizo hilo leo asubuhi majira ya saa 12 akiwa anajiandaa kuelekea mazoezini ndipo alipoona moshi ukifuka kutokea eneo la sebuleni kwake na aliposogea alibani ni moto ulikuwa ukiwaka.
"Nilisikia hewa nzito ndani, nikaamka kuelekea sebuleni, nilipofika nilikuta moto umetanda chumba kizima ndipo majirani walijitokeza na kuanza kutusaidia kuzima moto huo kwa kuvunja madirisha ya vioo na kumwaga maji ili moto huo uzime" alisema Niyonzima
Nashukuru tulifanikiwa kuuzima moto baada ya muda kwa kushirikiana na majirani lakini vitu vyote vilivyokuwa ndani hatukufanikiwa kuivitoa vikiwa salama, baadhi ya vitu vilivyoungua ni pamoja na Luninga iliyokua imefungwa ukutani, redio (music system), makochi na fenicha za ndani.
Aidha Niyonzima amesema moto huo utakua umetokana na shoti ya umeme juu ya dali kwani ndio sehemu inayooenekana kuwa chanzo cha moto.
Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Baraka Kizuguto alifika nyumbani kwa Niyonzima majira ya saa 2 kasorobo asubuhi kuongea na mchezaji ambaye alisema anashukuru familia yake wote wako salama na hakuna aliyedhurika zaidi ya vitu vilivyoteketea na moto.
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unampa pole Niyonzima kwa matatizo yaliyomfika, Mungu amjalie nguvu na uvumilivu na kusema upo nae pamoja katika wakati huu mgumu.
No comments:
Post a Comment