Kitale |
MUIGIZAJI Kitale ‘Rais wa Mateja’, ameweka wazi kuwa anaichukulia fani yake ya uigizaji kama ajira, na kuwashangaa wale wote wanaomdharau kutokana na kuigiza kama ‘teja’.
Alisema ameitumia fursa ya kuishi karibu na watumiaji wa dawa za kulevya kwa kujitengenezea ajira huku akiwashangaa wanaopitwa na nafasi kama hizo.
“Mwigizaji mzuri ni yule anayefanya kitu tofauti, ndivyo nilivyofanya mimi, mwanzoni wakati naanza watu wengi walishindwa kuona nitakapofikia lakini, sasa nipo hapa, naingiza pesa na mwigizaji mwenye mafanikio na ushawishi mkubwa,”alijisifu Kitale.
Alifafanua kuwa pamoja na kuwa anaswali kama wanavyofanya waumini wengine na hajawahi kunywa hata pombe, amemudu kuigiza katika nafasi hiyo ngumu, hivyo wanaomcheka na kumdhihaki wajipange upya.
“Kama unavyoniona napiga pamba, nina mke na familia yangu inaishi kijanja mjini hapa, bado nina heshima kama msanii anayejua maana ya sanaa,”alisema Kitale.
No comments:
Post a Comment