Jack Welshere |
LONDON, ENGLAND
YAMEFUNGWA mabao mengi katika Ligi Kuu England kuanzia Agosti mpaka leo Alhamisi mwisho wa mwezi wa Oktoba. Lakini yafuatayo yanaweza kuwa mabao bora zaidi
.
Sone Aluko vs Newcastle United
Bonge la bao! Huku matokeo yakiwa 2-2, Hull City ilikuwa ikisukumana na Newcastle katika uwanja wao wa nyumbani St. James’ Park. Shuti kali la mbali la Sone Aluko lilikwenda moja kwa moja katika kona ya nyavu za Newcastle. Bonge la bao, na ndio lilikuwa la ushindi huku likiwa tofauti pekee kati ya timu hizo.
Aguero vs Manchester United
Ni kama lile la Aluko, lakini hili lilikuwa bora kidogo. Kulikuwa na muvu nzuri katika upande wa kushoto ambayo iliwajumuisha Samir Nasri na Aleksander Kolarov, mwishowe krosi murua ya Kolarov ilimfikia Aguero ambaye aliupiga mpira kwa umaridadi kwa shuti dhaifu ambalo lilimpita De Gea.
Ravel Morrison vs Tottenham
Akiwa ameuchukua mpira katikati ya uwanja, ilionekana kama vile Morrison hakuwa na madhara.
Alikatiza katikati ya wachezaji watatu wa Tottenham huku akiwa anaangaliwa tu na mabeki kabla hajaunyanyua mpira kumvuka kipa Hugo Lloris kwa umaridadi. Bonge la bao na ndio lilikuwa bao la tatu katika ushindi wa 3-0 wa West Ham ugenini kwa Tottenham.
Wilshere vs Norwich City
Hili lilikuwa bonge la bao. Bao la kitimu hasa! Ni aina ya bao la Arsenal halisi. Santi Cazorla alingia na mpira akitokea kulia na kumpasia Wilshere ambaye alipigiana pasi mbili za haraka haraka na Olivier Giroud.
Wakati huo, Giroud alikuwa anatumia kisigino zaidi na pasi ya mwisho kwenda kwa Wilshere ilikuwa tamu. Alifunga kwa shuti dhaifu la mguu wake wa kulia
Pajtim Kasami vs Crystal Palace
Moja kati ya mabao bora duniani. Bao la Kasami lilikuwa zuri sana. aliupokea mpira mrefu kwa kifua akauangusha mbele yake, lakini kabla haujagusa chini alipiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni. Bonge la bao na hakuna kocha anayeweza kufundisha kile ambacho Kasami alikifanya
No comments:
Post a Comment