LONDON, ENGLAND
KOCHA Mkuu wa zamani wa Sunderland, Paolo Di Canio ameripotiwa kuwahi kuamrisha basi la timu hiyo liondoke na kumwacha nyota wao mpya, El-Hadji Ba wakati walipokwenda kumenyana na Crystal Palace kwenye Ligi Kuu England.
Mtaliano huyo, ambaye kwa sasa amefukuzwa Sunderland baada ya kuboronga vibaya ameelezwa alipoteza ushirikiano na wachezaji wake ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Na sasa imeibuka kwamba Di Canio aliamuru basi la timu liondoke na kumwacha nyota wake waliyemsajili katika majira ya kiangazi wakati walipokwenda Selhurst Park ambapo walikumbana na kipigo cha mabao 3-1.
Kisa cha Ba kuachwa ni kwamba alirudi nyumbani hotelini kuchukua begi alilokuwa amelisahau, kwa mujibu wa Daily Mail. Ripoti zimebainisha kwamba mchezaji huyo alilazimika kuomba lifti ili kufika uwanjani.
Wiki iliyopita straika wa Sunderland, Steven Fletcher alidai kwamba kocha huyo alikuwa akiwakataza kucheka au kutabasamu walipokuwa mazoezini.
No comments:
Post a Comment