Tuesday, 15 October 2013

BUNDI KUKWAMISHA UJENZI WA UWANJA WA LIVERPOOL

Muonekano wa uwanja wa Aflied wa Liverpool.

Bundi wanaelekea kukwamisha mipango ya kuendeleza uwanja wa Anfield unaomilikiwa na Liverpool.


Wakati Liverpool wakiimarisha timu yao na inafanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya England (EPL), klabu inajiimarisha kwa kuongeza uwezo wa uwanja huo ili uchukue washabiki 60,000.

Hata hivyo, mipango inayowasilishwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Liverpool inaweza kukataliwa kwa sababu maeneo panapotakiwa kutanuliwa uwanja ni mazalia ya bundi.

Mamalia hao wanaoruka wamekuwa wakionekana Anfield na wataalamu wanasema itakuwa vigumu kuendeleza uwanja kwa kuupanua kwani kutaathiri viumbe hao.

Sheria za England pamoja na zile za kimataifa zinalinda maslahi ya bundi kama moja ya viumbe wasiotakiwa kuathiriwa.

Wakuu wa Liverpool wamedai kwamba hawajui kama kuna mazalia ya bundi katika uwanja wao lakini iwapo wana ikolojia watabaini kuwapo mazalia yao, itabidi waachiewe sehemu katika eneo ambalo uwanja ungepanuliwa, maana sheria inasema hivyo.

Hata Liverpool walipocheza na Notts County mwezi uliopita, washabiki walionekana wakinyoosha vidole vyao kuelekea bundi walikokuwa wakipiga piga mabawa yao na kuruka juu ya vichwa vyao.

Hiyo ilikuwa wakati vijana wa Brendan Rodgers wakicharuka na kufunga moja ya mabao yao manne katika mechi ya Kombe la Ligi.

Jioni ya siku hiyo hiyo, bundi alionekana akiruka kwenye eneo la mbele ya majengo ya Anfiled wakati washabiki wakielekea kwenye milango kutoka nje kwenda makwao baada ya mechi.

Ni hali hiyo inayotia shaka kwamba ndoto za Liverpool kuufanya uwanja wao ubebe watu 60,000 zitatimizwa.
Je, kipi cha muhimu – maendelezo ya uwanja au bundi? Sheria inasema bundi wasibughudhiwe kwa jinsi yoyote na wana Liverpool wanataka kuona uwanja mkubwa zaidi.

Itakumbukwa kwamba wamiliki wapya wa klabu hiyo walitangaza kwamba walifuta mipango ya kuhama kutoka Anfield kwenda eneo jingine muda mfupi baada ya kuitwaa klabu.

Hali hii itawaweka njiapanda wadau wa Liverpool wakati huu ambapo Mapinduzi Mekundu chini ya Kocha Rodgers yanashika kasi, ambapo Liverpool walianza kwa kuwafunga Manchester United na wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamefungana na Arsenal kwa pointi.

No comments:

Post a Comment