Monday, 30 September 2013

KUELEKEA USIKU WA UEFA,WENGER AZUNGUMZIA HALI YA MAMBO NDANI YA ARSENAL

Arsene Wenger

Kuelekea michezo ya keho kwenye ligi  ya mabingwa kocha wa Arsenal,Arsenal Wenger ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Napoli anaanza kwa kusema,,

'Watu wanasema ili kufuzu raundi ya mtoano unahitaji wastani wa pointi 10.2 kwangu tayari nimeshapata wastani wa point 2,

Kumhusu Benitez anaendelea kusema,

Ni kocha bora duniani na ana uwezo mkubwa unapocheza na timu yake huwezi ukasema unakwenda kushinda moja kwa moja yote yanaweza kutokea

Kuhusu kiwango cha Giroud,,

Kwa sasa anazidi kuimarika wakati anakuja hapa msimu uliopita hakuwa kwenye kiwango bora lakin kwa sasa umri(26) unavozidi kwenda ndivyo anavyozidi kuimarika  

Kuihusu timu ya Napoli

Wana mchezaji mzuri kama Insigne lakini naamini Sagna atamthibiti vizuri

Kumhusu Rosisky

Anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada a kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua

Kuhusu Flamini

Amefanya mambo kuwa sawa sawa(team balance) 

No comments:

Post a Comment