Monday, 16 September 2013

HATA MJUKUU WANGU ANGEMUONEA HURUMA KAGAWA


Shinji Kagawa
Akili yangu inafikiria mbali na kujiona kama nimeshazeeka alafu nimekaa na mjuu wangu mwenye miaka 3 kwenye sofa zuri huku yeye akiwa ameweka miguuu juu ya meza huku mkono wake wa kulia umeshikila glasi ya maziwa na kunywa kama hataki.,,

Alafu wakati huo tunaangalia habari ya michezo kutoka Skynews mara anaonekana Shinji Kagawa akiongea kwa hisia jinsi anavyohitaji kucheza Manchester United lakini hapewi nafasi mbaya zaidi akirudu inchini kwake Japani anaonekana star wa timu.
Hapa hata ungekuwa wewe lazima ungeumia tena maumivu ya hisia yanayokaribia ya mapenzi,Habari hii inazidi kuwa na maswali mengi zaidi hasa pale Kagawa anapoulizwa swali na mwandishi mmoja baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu yake ya taifa,kwa nini huchezeshwi mara kwa mara kwenye kikosi cha Man U,Kagawa anajibu,’kamuulize Moyes kwa nini sichezi’
Unaweza ukajiuliza inamaana Kagawa alishindwa kutoa majibu ya swali hilo au hajui kama hachezeshi,anamuogopa Moyes au anaipenda sana Man U hivyo hata kama ikimfanyia jambo ambalo linauumiza moyo wake basi anaitetea.Majibu ya uhakika anayo Moyes lakini moyo wa Kagawa unazidi kugawanyika viande vipande kwa maumivu anayoyapata.
Baada ya mjukuu wangu kuiona hii habari na kuyaona machozi yakikaribia kutoka kwenye macho ya kagawa ananiuliza,Babu mbona Yule mzungu anataka kulia au kuna mtu amempiga,mimi naanza kumjibu unaijua timu inayoitwa Manchester United,ile ya yule mzee anaependa kutafuna Big G,haswa mjukuu wangu,yule mchezaji unaemuona ni mchezaji wa hiyo timu.Sasa kwa nini anataka kulia au kafukuzwa kwenye hiyo timu,Najisikia kucheka lakini najizuia nahisi nitamuumiza mjukuu atahisi namcheka.
Nazidi kuyafikiria mazungumzo ya mimi na mjukuu wangu yatakavyokuwa,unajua mjukuu wangu kila mtu anaefanya kazi kwenye hii dunia anahitaji kuwajibika katika kazi yake ili imletee mafanikio anayoyahitaji,kama mtu ni mwalimu anahitaji  kufundisha tena wanafunzi wafaulu hiyo ndio furaha yake,kama mtu ni mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara mwisho wa yote imleteee faida na kama mtu ni mchezaji  basi anahitaji kucheza.
Huyo mtu uliemuona kwenye Tv ni mchezaji hivyo nanahitaji kucheza,sio mara moja kwa mwezi bali kila mara timu yake inaposhuka uwanjani akiwa na kikosi cha kwanza hilo ndilo shauku la moyo wa huyo mtu.Jambo kubwa linalomfanya awe na huzuni ni kwa sababu klabu yake ya Manchester United haimchezeshi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.
Wakati mchezaji huyu anakuja Man U 2012 akitokea Borussia Dortmund,alikuwa ni mchezaji nyota wa klabu hiyo,alikuwa na maisha alikuwa anayataka katika soka,kila mfuatiliaji wa soka alimfahamu,uwezo wake wa kuichezesha timu muda wote wa dakika 90 na kutoa pasi za magoli(assist pass).Hii ilizidi kumfanya atambulike kwa kila mtu na hata makocha wa timu nyingine kummezea mate.
Hivyo akili nyingi za Ferguson zilimsajili na moyo wake uliamini alichokuwa anakifanya kwenye ligi ya Ujerumani basi ndicho atakachokifanya na hata kuzidisha  akiwa England.Ferguson alizidi kuvuta hisia jinsi magoli yatakavyokuwa yakitengenezwa kwa wingi hasa ukuzingatia ndo alikuwa amempata Robin Van Persie kutoka Arsenal,lakini mambo yamebadilika huyu sio yule kagawa wa dakika 90,huyu hata benchi wakati mwingine hakai pale Old Traford kwa nini moyo usiumie kwa hali kama hii.

Kagawa hafanyi kile alichokuwa anakifanya Bungesliga,haonekani kwenye Tv za wajapan kama alivokuwa akionekana akiwa Dortmund,wajapan wanaishia kulipa viingilio vya Dstv zao bure kwa kumuangalia Welbeck wakati wao wanamhitaji Kagawa.Ndio maana Kagawa anahuzuni moyoni mwake,anaumia zaidi anapomuona Ashely Young akitokea kwenye majeraha na kuingia kwenye mfumo wa kocha David Moyes,maumivu yanaongezeka zaidi anapomuona kocha mchezaji Ryan Gigs akipewa nafasi kuliko yeye.Hapa ndipo mjukuu wangu anamuonea huruma Shinji Kagawa.   

No comments:

Post a Comment