CM Punk akiwa amembeba Randy Orton |
Daniel Bryan, CM Punk na Big Show wote wanatarajiwa kupambana wiki hii kwenye usiku wa WWE Late Night Raw..
Usiku wa mieleka ulimshudia bingwa wa mchezo huo Randy Orton akipoteza ubingwa wake kwa kupigwa na Daniel Bryan.
Lakini swali linakuja ni kwa namna gani anaweza kuulinda ubingwa huo mbele ya wapiganaji kama Tripple H,Big Show,Cm Punk na wengine.
Big Show ndio yupo karibu kupigana nae ikiwa atapita katika mzungukowa mwisho wa kwa kupambana na Dean Ambrose katika US Champion na kama atashinda atapata nafasi ya kwenda kupambana kwenye fainali kwa ajili ya kugombania ubingwa wa WWE.
CM Punk nae amerejea mchezoni baada ya kupata kipigo kilichopelekea maumivu ya kukaa nje ya uwanja kwa muda kutoka kwa rafiki yake Paul Heyman.
Mpiganaji wa zamani wa mchezo wa mieleka Dusty Rhodes anatarajiwa kuonekana Lve kwenye uwanja wa RAW baada ya kukubali ombi la kufanya matangazo ya kibiashara na mmoja ya watu wenye hisa kubwa kwenye mchezo huo Stephanie McMahon.
No comments:
Post a Comment