Thursday, 15 May 2014

Marcelo afichua siri ya utotoni




BEKI Mbrazili, Marcelo, amefichua kwamba ilibaki kidogo aachane na soka na asingeweza kujulikana kwenye ulimwengu wa mchezo huo kama si juhudi za babu yake.
Staa huyo wa Real Madrid alisema ushawishi wa marafiki zake waliokuwa wakipenda starehe nusura umponze na kuwaiga kitu ambacho kisingekuwa na mwisho mzuri kwa maisha yake ya soka.
“Nilitaka kuacha soka nilipokuwa na umri wa miaka 15. Kipindi hicho nilikuwa nikitaka kwenda kwenye starehe na marafiki zangu. Maisha nilianza kuyafahamu tangu nikiwa mdogo sana,” alisema.
“Bahati nzuri babu yangu alinizuia. Aliniambia nina uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira. Mwanzoni sikumwamini.”
Katika mahojiano, Marcelo, aliongeza: “Nikiwa mtoto nilitaka kuwa mtu wa kuzima moto kama alivyokuwa baba yangu. Namwona kama shujaa kwangu.”
Beki huyo wa pembeni alisema kitu ambacho kinamuumiza moyo kwenye soka ni kuona wenzake wanafunga mabao mengi wakati yeye anashindwa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment