Thursday, 27 March 2014

Scholes awawakia mastaa Arsenal


KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Mwingereza Paul Scholes, amesema Arsenal ipo umbali wa maili moja kukaribia ubingwa wa Ligi Kuu England.
Akizungumza baada ya Arsenal kupoteza uongozi wake wa mabao 2-1 na kutoa sare ya mabao 2-2 nyumbani mbele ya Swansea City, Scholes aliwashambulia viungo Mikel Arteta, Santi Cazorla, Tomas Rosicky na Mesut Ozil kwamba hawachezi kwa kujituma na hilo linaifanya timu kuwa kwenye wakati mgumu wa kupata ushindi.
Baada ya kipigo cha mabao 6-0 kutoka kwa Chelsea wikiendi iliyopita, wengi waliamini Arsenal ingezinduka dhidi ya Swansea uwanjani Emirates, lakini badala yake ilichemsha na kufanya vibaya.
“Ni mashabiki wa Arsenal ninaowaonea huruma, kwa sababu mambo yamekuwa yale yale kila mwaka,” alisema Scholes.
“Wanaonekana kuwa na uchu wa taji, lakini wanapoingia uwanjani hakuna kitu. Mashabiki wana hamu ya ubingwa, lakini ukweli timu hiyo ipo umbali mrefu sana wa kulifanikisha hilo. Wanahitaji kupambana na kuwa na viongozi uwanjani.”
Scholes alisema Arsenal haitatwaa taji lolote la Ligi Kuu kwa miaka ya hivi karibuni hadi hapo itakapopata wachezaji vinara wenye kupambana kama ilivyokuwa enzi za manahodha, Patrick Viera na Tony Adams.
“Hawa wachezaji kama Arteta, Cazorla, Rosicky na Ozil, wanacheza tu. Hawana nidhamu uwanjani. Arsenal haina kiongozi kama wa enzi zile za Patrick Vieira, Tony 

No comments:

Post a Comment