'THE CLASS OF 92' WAKIONGOZWA NA BECKHAM NA GARY NEVILLE WARIPOTIWA KUTUMIWA NA FAMILIA YA KIFALME YA QATARI KATIKA UNUNUZI WA MANCHESTER UNITED
Ripoti kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali zinasema kwamba David Beckham na wachezaji wenzie waliokuwa wanaunda kikosi cha Man United mwaka 1992 kwa kushirikiana na kampuni ya kutoka nchini Qatar wapo katika harakati za kuinunua Manchester United.
Hata hivyo United wamekanusha taarifa kwamba wamiliki wa timu hiyo Familia ya Malcom Glazers imepoteza hamu ya kuendelea kuimiliki timu hiyo na sasa wanataka kuiuza.
Lakini mapema jana iliripotiwa kwamba David Beckham, Gary na Phil Neville, Ryan Giggs, Nicky Butt, na Paul Scholes, wamekuwa wakitumika na familia ya kifalme ya Qatar katika mpango huo wa kuinunua United.
The Glazers - ambao wanaimiliki United kwa 90% - wamekuwa wakiripotiwa kutaka kuiuza timu hiyo, huku mmoja wa watu wa karibu wa familia hiyo akikaririwa akisema kwamba "kila mtu anajua klabu inauzwa".
The Sun inaripoti kwamba familia ya kifalme ya Qatar imekuwa na mawasiliano na Glazers kuhusiana na dili la kuinunua timu hiyo lakini kikwazo kimekuwa kwenye bei.
Pia inasemekana Gary Neville - ambaye amefungua Cafe Football na Giggs mwaka 2013 - ndio mtu aliye nyuma ya wazo hilo.
No comments:
Post a Comment