KIUNGO, Emmanuel Frimpong ametoa kali baada ya kudai uhamisho wake Barnsley utapunguza kasi ya kuwanasa mademu kwa kuwa klabu hiyo si maarufu sana.
Staa huyo wa Ghana, aliyeondoka Arsenal kwenye usajili wa mwezi uliopita alikuwa akiitumia timu hiyo kwa faida ya kuwanasa mabinti wazuri licha ya kwamba hakuwa akipata namba.
Kwenye kikosi cha Arsenal, Frimpong amecheza mechi 16, huku akiandamwa na majeruhi na kuibuka kwa Jack Wilshere kumemfanya akose namba klabuni hapo.
Lakini, baada ya kuhama Arsenal na kutimkia Barnsley, Frimpong aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba atawezaje kuwapata tena mabinti akiwa na klabu ya daraja la chini.
“Nitawapate mabinti tena,” aliandika Frimpong kwenye ukurasa wake wa Instagram, lakini ujumbe huo aliufuta haraka sana. Kwenye kikosi cha Barnsley, Frimpong alianza vibaya baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wake wa kwanza baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kumchezea rafu mbili mchezaji mmoja ndani ya dakika saba.
No comments:
Post a Comment