KOCHA, Carlo Ancelotti amesema uamuzi wa klabu yake ya Real Madrid kumpiga bei kiungo Mesut Ozil kwenda Arsenal ni kosa kubwa sana ambalo limewahi kufanyika.
Kwenye mjadala huo Ancelotti alisema anahusika pia kwenye kubeba lawama za supastaa huyo kuondoka Santiago Bernabeu na kutua Emirates katika usajili wa majira ya kiangazi uliofanyika mwaka jana.
Ancelotti alisema: “Nadhani nilifanya makosa wakati nilipomruhusu aondoke.
Lakini, kauli ya Ancelotti inaonekana kutibua mambo Madrid kwani baadhi ya maofisa wa klabu hiyo wanasisitiza Ozil hakuwa na umuhimu wowote katika klabu yao.
Katika kuweka mambo sawa, Ancelotti alisema kilichotokea ni kwamba wanamkumbuka mchezaji huyo katika hali ya kawaida tu.
No comments:
Post a Comment