Michuano ya Tennis kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 16 ukanda wa Afrika Mashariki inaanza hapo leo jijini Dar es Salaam Tanzania ikishirikisha timu 8.
Timu zinazotaraji kushiriki ni wenyeji Tanzania, Rwanda,Burundi,Kenya,Seychelles, Comoro, Ethiopia, na Sudan.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Tennis Tanzania,Bi Fina Mango ambaye pia ni Mkurugenzi wa mashindano hayo amesema kuwa Michuano ya Mwaka huu mbali na kuongezeka idadi ya Timu zinazoshiriki yaani timu 8,lakini pia timu zitakazoshika nafasi tatu za juu zitafuzu kushiriki michuano ya Afrika ya mchezo huo inayotaraji kufanyika nchini Kenya baadae mwezi March mwaka huu.
Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mchezo huo ITF Bwana Thierry Ntwali kutoka Burundi amesema juhudi zimekuwa zikifanyika kuinua mchezo wa Tennis katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo amesema hivi sasa nchini Burundi kumeanzishwa Kituo cha Kimataifa cha kuwaendeleza Vijana chipukizi wanaoonyesha Kipaji katika Mchezo huo,huku Michuano ya Mwaka huu inayoanza hapo kesho ikitaraji kuibua Vipaji vipya.
Kwa upande wake Kocha msaidizi wa Timu ya Tennis ya Tanzania Nicholas Jonas amesema wachezaji wake wamejiandaa Vema kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo ambayo mwaka Uliopita Timu ya Tanzania ilishika nafasi ya Pili na kwa kuwa wachezaji wengi ni wale wale waliocheza mwaka uliopita basi mwaka huu ni nafasi yao ya kutwa Ubingwa wa Michuano hiyo inayotaraji kuanza kesho tarehe 12 hadi tarehe 19 mwezi huu wa January 2014.
No comments:
Post a Comment