Friday, 17 January 2014

Jose atumia mbinu kumvuruga Moyes


KOCHA, Jose Mourinho ameanza chokochoko akitaka kumpumbaza David Moyes baada ya kudai kwamba amepata taarifa kutoka ndani ya Manchester United kwamba kwenye timu hiyo mambo si mazuri.
Mourinho ameibuka na maneno hayo akitaka kumvuruga Moyes ambaye Jumapili hii timu zao zitamenyana kwenye mechi ya Ligi Kuu England uwanjani Stamford Bridge. Madai ya Mourinho ni kwamba amezungumza na kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson na amemwambia kwamba maisha ndani ya klabu hiyo ni magumu sana.
Mourinho alisema: “Hisia zangu na baada ya mawasiliano niliyofanya na Sir Alex, Manchester United hawana furaha, japo wametulia. Wanamwamini David. Na David anawaamini pia. Sidhani kama yupo kwenye presha kubwa. Presha ni kitu kinacholetwa na vyombo vya habari kutokana na matokeo kuwa mabaya. Lakini, ubaya wa hilo ni kwamba presha haipo nje tu, ipo ndani pia.”
Moyes amekuwa na mwanzo mbaya katika maisha yake na kikosi cha Manchester United baada ya timu yake kushika nafasi ya saba huku ikiwa pointi tano pungufu kwenye nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mourinho alikuwa akipewa nafasi ya kurithi mikoba ya Ferguson wakati aliporipotiwa kustaafu Old Trafford kabla ya kibarua hicho kuchukuliwa na Moyes na yeye kutua Chelsea akitokea Real Madrid.
Alikuwa swahiba mkubwa wa Ferguson na wawili hao walikutana kwenye Hoteli ya Lowry jijini Manchester na kunywa kahawa kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City msimu uliopita, wakati huo akiwa na kikosi cha Los Blancos.
Mourinho ameanza kumvuruga Moyes kabla ya kuvaana naye kwa kudai kwamba kikosi chake hakipo sawa baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani wa klabu hiyo ambaye hakumtaja

No comments:

Post a Comment