MJADALA kuhusu kipaji kwamba mtu anazaliwa nacho au anakipata kwa kujifunza, bado ni gumzo nchini Nigeria.
Hiyo inatokana na watu wengi kuwa na mtazamo tofauti hasa kwa mwigizaji kama Mercy Johnson aliyekuwa na uwezo wa kuigiza nafasi yoyote na kuicheza kwa ufanisi mkubwa kuliko mwigizaji mwingine wa Nollywood.
Kwa mwaka 2013, mtengenezaji wa filamu, Charles Novia, tayari amemtaja Mercy kuwa ni mwigizaji bora wa kike nchini humo akisema hakuna aliyeweza kuigiza kwa umahiri wa kiasi chake.
“Mercy Johnson ni jembe, si mwigizaji wa kawaida. Ni kati ya waigizaji wachache walioweza kushikilia nafasi zao tangu walipoanza kuigiza hadi sasa,” anasema Novia.
No comments:
Post a Comment