Saturday, 7 December 2013

KOCHA AIPA TAIFA STARS UBINGWA CECAFA





KOCHA wa zamani wa Harambee Stars, Zedekiah Otieno, amesema kama si Kenya itakayotwaa ubingwa wa Cecafa Senior Challenge Cup, basi taji hilo linaweza kwenda Sudan au kubaki kwa Waganda.
Otieno ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Sony Sugar, amesema mataifa hayo yaliyofuzu robo fainali zinazoanza leo Jumamosi ndio wameonyesha soka lenye matumaini.
“Timu hizi zimeonyesha mchezo wa kiufundi na nidhamu ya hali ya juu hadi kufikia kwenye hatua za sasa,” alisema.
“Zinafahamu jinsi ya kushinda michuano na pia zinafurahia baadhi ya wachezaji wenye viwango vizuri, tumeyaona hayo katika mechi zao zilizotan gulia.”
Hata hivyo ameonya kwamba, kikosi cha nyumbani kitarajie mechi ngumu zaidi kwenye robo fainali dhidi ya Rwanda huku akikitaka kiwe makini zaidi.
“Ninafahamu mashabiki wa nyumbani wanatarajia makubwa kutoka kwa timu ya nyumbani ingawaje Harambee Stars haikujiandaa vyema, hivyo kutokana na hilo watarajie kuwa na kipindi kigumu,” alisema.
“Ila nina imani nao kwa kuwa wameonyesha kuimarisha mchezo wao kutoka mechi moja hadi nyingine,. Ni timu
ambayo sasa inaweza kuwaletea kitu cha maana Wakenya kama itaamua kufanya hivyo. Nadhani wameshaamua.”
Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stars, James Nadwa,
amesisitiza kuwa hana hofu na vijana wake akishikilia kuwa wapo tayari kukabiliana na timu yoyote na kushinda.
Alisema wamekuwa wakiyafanyia kazi makosa yao katika kila baada ya mechi na ndio maana timu inaimarika.
Aliwataka mashabiki kufurika kwa wingi katika mechi yao ya robo fainali ili kuwatia hamasa vijana wake.

No comments:

Post a Comment