SUPASTAA wa Ghana, Kevin-Prince Boateng na mchumba wake mwanamitindo wa Kitaliano, Melissa Satta, wamebainisha kuwa wanatarajia kupata mtoto.
Wapendanao hao wanaofahamika kwa jina la ‘Satteng’ baada ya kuunganisha majina ya ubini wao, walichumbiana katika sherehe ya siri iliyofanyika mapema mwaka huu jijini Milan, Italia.
Taarifa za kwamba wawili hao wanatarajia kupata mtoto si tetesi tena baada ya kubainisha wazi kupitia mtandao wao wa kijamii wa Twitter.
Staa huyo wa Schalke 04 na Black Stars aliandika: “Tunafurahi kuwaambia kwamba kuna mwanafamilia mwingine kwenye ‘Satteng’ yupo njiani. Penzi kubwa kwake, Melissa na mimi.”
No comments:
Post a Comment