Kocha wa Simba Abdalla King Kibadeni |
KOCHA Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema wachezaji vijana William Lucian ‘Gallas’, Said Ndemla, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Ramadhani Singano ‘Messi’ ndiyo walikuwa roho ya timu hiyo mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.
Simba wamemaliza mzunguko huo wakiwa nafasi ya nne na pointi 24 nyuma ya Yanga inayoongoza na pointi 28, Azam ya pili na pointi 27 sawa na Mbeya City ambayo ni ya tatu.
Kibadeni alisema: “Nilikuwa mgeni na vijana walikuwa wengi, niliambiwa kazi yangu ni kutengeneza timu kwanza na suala la ubingwa baadaye. Sikuwa nawajua vizuri wachezaji, lakini kwa sasa namfahamu kila mmoja na ubora wake, hata nikipanga timu najua atakayefaa sehemu gani tofauti na nilipoanza,”alisema.
“Kwa jinsi ninavyowafahamu wachezaji kwa sasa kama nitaendelea na timu hii mzunguko wa pili, tutafanya makubwa, wachezaji vijana ndiyo wamefanya vizuri zaidi ya wakongwe.
“Kwanza niliwapa heshima wazoefu, na kama mlivyowaona watoto ndiyo waliong’ara, kama, Gallas na Ndemla .’’
Uongozi Simba umekuwa haufurahishwi na mwenenedo wa timu hiyo na kuna habari kuwa watapeana mkono wa kwaheri na kocha huyo.
No comments:
Post a Comment