![]() |
MWIGIZAJI wa filamu na mwanamuziki wa kizazi kipya, Snura Mushi, amedai kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Mrisho Ngassa wa Yanga.
Amedai kuwa alikuwa kimya bila kuzungumzia suala hilo, lakini ameona kuna baadhi ya watu wanataka kuhalalisha jambo hilo.
“Wapo wengi ambao najua watasema kuwa wacheza mpira ni mabwana zangu, lakini hakuna ninayetoka naye kimapenzi, mimi sitoki na Mrisho Ngassa ila nimefanya naye kazi ya filamu yangu ya Majanga, sasa watu wanatangaza kama Ngassa ni mtu wangu na natoka naye, lakini Ngassa ni msanii tu aliyeshiriki katika filamu yangu,”alidai Snura.
Snura alidai kuwa katika filamu yake ya Majanga, Ngassa kaigiza kama mumewe hivyo iwe kwa bahati mbaya au kuna mtu ambaye aliwaona katika baadhi ya picha na kutangaza kuwa ni wapenzi amekosea.
Msanii huyo ambaye anafanya vizuri katika filamu na muziki, nyota yake imeng’ara katika muziki na anatamba na wimbo wa ‘Nimevurugwa’.
No comments:
Post a Comment