Friday, 29 November 2013

RAMSEY NA WELSHERE WAPO VITANI



KOCHA Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema viungo, Jack Wilshere na Aaron Ramsey, wapo kwenye ushindani wa kuonyesha viwango vyao na hilo linamfurahisha kwa sababu litakuwa na manufaa makubwa kwa klabu.
Wilshere alifunga mara mbili wakati Arsenal ilipoinyuka Marseille mabao 2-0 juzi Jumanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na jambo hilo linamfanya Wenger kuamini Mwingereza huyo na mwenzake raia wa Wales wapo kwenye ushindani msimu huu.
“Wilshere ameanza kufikiria kwamba kile anachoweza kufanya Ramsey naye anaweza kukifanya pia. Amekuwa mtulivu anapokuwa mbele ya goli na bao lake la kwanza linathibitisha hilo,” alisema Wenger.
“Ni kama utani kuhusu Aaron, lakini hawa wawili ni viungo wanaopenda kufunga mabao. Ukweli sikuwahi kudhani kama Wilshere atakuwa mfungaji, lakini sina pingamizi. Kama nitakuwa nimekosea kwenye hili na Wilshere akawa mfungaji, nitafurahi

No comments:

Post a Comment