Kiungo mchezeshaji wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil ameondolewa katika kikosi cha timu yake y taifa kitakachicheza na England katka mchezo wa kirafiki usiku wa jumanne katika uwanja wa Wembley
.
Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa kwenye bench katika mchezo dhidi ya Italy ameondolewa kwenye kikosi sambamba na nahodha Philip Lahm na kipa namba moja Manuel Neuer.
Akizungumzia mabadiliko hayo kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema,"Mchezo dhidi ya England utakuwa ni wa mwisho kwa kutumia mbinu tofauti dhid ya wachezaji chipukizi na kubadilisha kikosi mara kwa mara,
Kwa wachezaji kama Ozil,Lahm na Neuer tayari wameshakuwa na uzoefu mkubwa,kwangu mimi nataka kuwapa nafasi hata wachezaji chipkizi hasa kwa mchezo dhidi ya timu kubwa kama Uingereza"
Ozil ambae anaongoza kwa kutoa pasi sita za magoli kakika klabu yake ya Arsenal na kuisaidia kukaa kileleni mwa ligi ya England na amekuwa akisumbuliwa na maumivu katika wiki hii .
Nae mlinzi Per Martesecker amejumishwa kwenye kikosi baaada ya kupona virusi vilivyokuwa vinamsumbua.
No comments:
Post a Comment